Kuna
wakati huwa tunajisikia vibaya na kujihisi kama kukata tamaa, kutokana na hali
ya kushindwa kutimiza malengo yetu kwa muda muafaka tuliojiwekea.
Najua
ni kitu ambacho wakati huwa kinauma hasa pale unapoona malengo yako hayatimii
upesi kama unavyotaka iwe. Je, ni kitu gani unachotakiwa kufanya hasa unaona
malengo yako hayajatimia kwa muda muafaka?
1.
Weka mipango yako upya.
Kama
mbinu ambazo umezitumia kufanikisha malengo yako hazijakusaidia kufikia malengo
yako kwa wakati, panga malengo yako tena upya. Acha kujiona umepoteza sana,
weka malengo yako upya na jaribu tena na tena na tena.
2.
Kuwa king’ang’anizi.
Pale
malengo yako yanaposhindwa kutimia kwa wakati jaribu kuwa king’ang’azi. Usije
ukaingia katika hali ya kukakata tamaa, kwa sababu hali ya kukata tamaa haiwezi
kukusaidia sana zaidi ya kukukwamisha tena.
3.
Hamasika na mafanikio ya wengine.
Hata
kama mambo yako yamekuwa magumu na malengo yako yameshindwa kutimia kwa wakati,
ili kurudi kwenye mstari jaribu kutumia njia ya kuhamasika kwa kuangalia
mafanikio ya watu wengine.
4.
Angalia changamoto zilizokuzuia.
Pia
ni kweli umeshindwa kufika pale ulipotaka kufika kwa wakati, sasa ni vyema
ukaangalia changamoto zile zilizokuzuia kufanikiwa. Ukishazitambua changamoto
hizo zinafanyie kazi mara moja na kisha songa mbele.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la
Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: