Kocha mkuu wa klabu bingwa Tanzania bara Young Africans, Hans van der
Pluijm, amesema hahofii chochote kuhusu mabadiliko ya benchi la ufundi
yanayozungumzwa na anaelekeza akili yake kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya
mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar .
Kesho jumatano Young Africans watakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar
katika mfululizo wa ligi kuu Tanzania Bara, mchezo utakaopigwa uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam ambapo Pluijm alisisitiza kuhusu kufahamu
umuhimu wa kushinda mchezo huo.
“Nimesoma kwenye magazeti jana na leo, lakini sijali hizo taarifa. Mwajiri wangu hajaniambia.
Na kuhusu mchezo wa kesho, Pluijm alisema awali alikuwa anajua ni Alhamisi, lakini jana ndiyo kaambiwa kwamba ni Jumatano.
Hata hivyo, Mholanzi huyo amesema hana namna nyingine zaidi ya
kujiandaa kwa mchezo huo ambao ni muhimu kushinda ili kurejesha imani ya
mashabiki katika mbio za kutetea ubingwa.
Habari za ndani kutoka Young Africans, zinaeleza kwamba benchi lote
la ufundi litavunjwa na zitakuja sura mpya kabisa baada ya mzunguko wa
kwanza wa ligi kuu.
Pluijm na wasaidizi wake, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma
Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wataondoka na Mzambia, George
Lwandamina atakuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Boniface Mkwasa, Manyika
Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: