Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba
amezipiga marufuku kamati za mazingira vijiji, vitongoji na kata
nchini kutoa vibali vya uvunaji wa misitu na kuzitaka zitambue wajibu
wao kuwa ni kulinda na kuhifadhi mazingira.
January
amesema sheria ya mazingira iko juu ya sheria nyingine hivyo
kuwataka waache kuidhinisha uvunaji na kuwapitishia watu vibali vya
kuvuna miti katika maeneo yao.
Amesema
kamati hizo zinatakiwa zitambue kuwa hazina mamlaka ya kupitisha
uvunaji wa miti na wala zisianzishwe kwa mtazamo wa utoaji wa vibari.
Amesema
kuna haja ya kuziwezesha kamati hizo kwa kuzipatia elimu juu ya
majukumu yao ambayo zinatakiwa zifanye kwa mujibu wa Sheria ya
Mazingira.
January
ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), amesema hairuhusiwi kufanya
shughuli zozote katika maeneo ya vyanzo vya maji badala yake ni
wajibu wa kila mtu kulinda na kuhifadhi vyanzo hivyo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: