Uamuzi
uliotolewa na Ukawa wa kutoshirikiana na Profesa Ibrahim Lipumba
hautaathiri umoja huo wa vyama vya upinzani katika uchaguzi wa umeya wa
manispaa za Dar es Salaam, baada ya madiwani wa CUF kumsusa.
Profesa
Lipumba anatambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis
Mutungi kwamba ndiye mwenyekiti halali wa CUF, hata pale mkutano mkuu
uliporidhia kujiuzulu kwake na kufuatiwa na uamuzi wa Baraza Kuu la
Uongozi kumfukuza uanachama.
Mgogoro
huo wa CUF uliokigawa chama hicho makundi mawili, uliwasukuma viongozi
wa Ukawa wakiongozwa na Freeman Mbowe kutoa tamko la kumtenga Profesa
Lipumba kwa madai kwamba analazimisha uenyekiti wa chama.
Licha
ya Profesa Lipumba kudai anaungwa mkono na wanachama wengi wa CUF,
madiwani wote wa chama hicho katika manispaa za Dar es Salaam
wametangaza kuiunga mkono Ukawa kwenye uchaguzi wa meya katika manispaa
zote.
Uchaguzi
wa meya unafanyika baada ya kuanzishwa kwa wilaya mpya za Ubungo na
Kigamboni. Ubungo imemegwa kutoka Wilaya ya Kinondoni na Kigamboni
imemegwa kutoka Wilaya ya Temeke.
Tayari
manispaa za Ubungo na Kinondoni zimegawana kata na kila moja itakuwa na
meya na uchaguzi unatarajiwa kufanyika wiki ijayo. Manispaa za Temeke
na Kigamboni bado hazijafikia mchakato wa kugawana kata na madiwani.
Madiwani
kadhaa wa CUF waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, kwa nyakati
tofauti walisema hawamuungi mkono Profesa Lipumba anayepinga Ukawa.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: