JITIHADA za Rais John Magufuli katika kubana matumizi yasiyo ya
lazima serikalini, ambazo alizihamishia katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC), ikiwamo kuzuia safari zisizo za lazima katika jumuiya
hiyo, zimewezesha kuokoa zaidi ya Sh bilioni 1.2.
Rais Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na
aliahidi kuchukua hatua za kubana matumizi yasiyo ya lazima na ikibidi
kutumbua watendaji wa EAC, baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo
Machi mwaka huu jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Liberat Mfumukeko alisema jana jijini hapa
kuwa jitihada za kubana matumizi yasiyo ya lazima, zimeokoa Dola za
Marekani 588,768 (zaidi ya Sh bilioni 1.2) ndani ya kipindi cha miezi
mitatu kuanzia Mei hadi Agosti mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu ashike
wadhifa huo Aprili mwaka huu, Balozi Mfumukeko alisema kiasi hicho cha
fedha kiliokolewa kutokana na kubana safari zisizo za lazima za
watumishi na watendaji wa jumuiya katika kipindi hicho.
“Utekelezaji wa ubanaji wa matumizi yasiyo ya lazima unategemewa
kuokoa dola za Marekani milioni sita kwa mwaka huu wa fedha 2016/2017 na
tutakuwa tunatoa taarifa hizi kwa watu wa Afrika Mashariki kila baada
ya muda,” alisema Balozi Mfumukeko ambaye ni Katibu Mkuu wa Tano wa EAC.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: