Maadhimisho ya miaka
17 ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika jana
mjini Bariadi mkoani Simiyu jana bila kuwapo wa familia ya mwasisi huyo
wa Taifa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema Oktoba 5, mwaka huu Mama Maria
Nyerere alikuwa miongoni mwa waalikwa katika sherehe hizo na mipango
kwa ajili ya malazi yake na msafara ilikuwa imeandaliwa.
Katika
mipango ya awali, mama Maria na msafara wake alipangiwa kufikia katika
nyumba za halmashauri ya mji wa Bariadi zilizoko eneo la Nyamuata kabla
ya kuhamishiwa katika hoteli mpya ya Sumayi
katikati ya mji wa Bariadi.
Meneja
wa hoteli hiyo, Mabula Mapolu alithibitisha ugeni wa Mama Maria
kupangiwa kufikia hotelini lakini, baadaye walipewa taarifa kuwa ugeni
huo usingefika na badala yake
hoteli
hiyo ikapangiwa wakuu wa mikoa na wilaya kutoka Zanzibar, ambao nao
walilazimika kuondoka juzi kutii agizo la Rais John Magufuli la kuwataka
kurejea kwenye vituo vyao vya kazi.
Akizungumzia sababu za familia hiyo kutofika, mmoja wa watoto wa Mwalimu Nyerere, Madaraka
Nyerere
alisema yeye binafsi hakuona mwaliko wa familia kuhudhuria sherehe
hizo, akisema huenda ulipokewa na mwana familia mwingine kwa kuwa
familia yao ni kubwa.
“Yawezekana mwaliko ulipokewa na mmoja wa wanafamilia kutokana na familia yetu kuwa kubwa. Lakini aliyeupokea akapata hudhuru na
kushindwa kuhudhuria; Hii haimaanishi kuwa Serikali haikutoa mwaliko,” alisema Madaraka akiwa Butiama.
Familia
hiyo jana ilishiriki ibada maalumu katika Kanisa Katoliki Butiama
ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi kadhaa wa Serikali, wakiwamo Mkuu wa
mkoa huo, Dk Charles Mlingwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo aliyetajwa kumwakilisha Rais John Magufuli pamoja na
wakuu wa wilaya za mkoa wa Mara.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: