Katibu
mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye amekuwa kimya kuzungumzia
sakata linaloendelea ndani ya chama hicho likimuhusisha Profesa Ibrahim
Lipumba, jana aliondoa ukimya na kueleza kuwa kinachoendelea ni mpango
ulioandaliwa wa kuvuruga jitihada za chama hicho za kudai haki, lakini
hautafanikiwa.
Pamoja
na hayo, Maalim Seif, aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais katika
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), amesema kuna jitihada alizoziita za
mwendokasi za jumuiya ya kimataifa kutatua mgogoro wa kisiasa visiwani
Zanzibar.
Maalim
Seif alisema hayo jana wakati akitoa salamu zake fupi kwa mamia ya
waumini na wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika Msikiti wa
Kihinani, Wilaya ya Magharibi A.
CUF
iko kwenye mvutano wa uongozi kutokana na Profesa Lipumba kushika ofisi
kuu za chama hicho zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam akisema kuwa
ndiye mwenyekiti halali wa chama hicho baada ya Msajili wa Vyama vya
Siasa nchini kutoa msimamo na maoni ya ofisi yake kuhusu sakata hilo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: