Chama cha soka nchini England (FA), kimetoa tahadhari kwa viongozi wa
klabu za Liverpool na Man Utd kwa kuwataka wawakanye mapema mashabiki
wao kuelekea katika mchezo wa siku ya jumatatu ambao utachezwa kwenye
uwanja wa Anfiled.
FA wametoa tahadhari hiyo kwa kutumia kigezo cha vurugu
zilizojitokeza wakati timu hizo zilipookutana mwezi Mei kwenye michuano
ya kombe la Europa League, na kupelekea shirikisho la soka barani Ulaya
UEFA kuzitoza faini ya Euro 40,000 sawa na Paundi 30,565, kufuatia
vurugu zilizojitokeza katika michezo miwili ya hatua ya mtoano
iliyochezwa Old Trafford na Anfiled.
Katika michezo hiyo mashabiki wa Liverpool waliwasha miale ya moto na
kuitupa sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Anfiled ili hali wale wa Man
utd walilipiza kisasi kwa kujazama katika kituo cha treni na kuzua
tafrani kwa watu wengine waliokua na nia ya kuwahi kufanya shughuli zao.
Hata hivyo pamoja na FA kutoa tahadhari hiyo, tayari mashabiki wa
pande zote mbili wameanza kuonyesha viashiria vya kuleta fujo kupitia
mitandao ya kijamii, na suala kubwa linalojadiliwa ni uteuzi wa mwamuzi
Anthony Taylor ambaye anadaiwa huenda akaibeba kwa makusudi Man Utd.
Kisingizo kikubwa kinachotumiwa na mashabiki wa Liverpool ni kwamba,
mwamuzi huyo alizaliwa mjini Manchester na kwa sasa anaishi maili sita
kutoka Old Trafford, hivyo inawaaminisha huenda akaamua kuipendelea timu
ya nyumbani kwao.
Mashabiki wa Man Utd wamekua wakipinga suala hilo na kuwataka
wapinzani wao kukaa mkao wa kula kwa kusubiri kichapo kama
walivyowafanya msimu uliopita, ambapo Liverpool walifungwa katika mchezo
wa nyumbani na ugenini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: