Taasisi ya T.Marc
Tanzania, ambayo iliendesha mashindano ya Dume Challenge imeeleza
kushtushwa na kusikitishwa na taarifa za kukamatwa kwa Salum Njwete,
maarufu kwa jina la Scorpion.
Taasisi
hiyo pia imethibitisha kuwa Njwete alishiriki na kushinda mashindano ya
Dume Challenge Season 1 mwaka 2012 na kuwa balozi wa kondomu za taasisi
hiyo chapa ya Dume kuanzia mwaka 2012 hadi 2014.
Njwete
alikamatwa na kushtakiwa kwa uporaji wa kutumia silaha na kumjeruhi
baada ya wananchi kulalamika kwenye vyombo vya habari kuwa kuna mtu
anayeitwa Scorpion aliyekuwa akipora na kujeruhi wananchi, akiwemo
kinyozi Said Ally wa Mabibo Hosteli aliyeporwa fedha na kutobolewa
macho.
“Hata
hivyo, tangu mwaka 2014, Bwana Njwete hajakuwa na uhusiano na chapa
hiyo,” inasema taarifa ya T-Marc iliyosainiwa na mkurugenzi mkuu, Diana
Monika Kisaka.
“T-Marc
pia inapenda kuthibitisha kuwa Bwana Njwete alikuwa balozi wa programu
ya kuwezesha wasichana ya “Hakuna wasichoweza” mwaka 2014 ambayo imeisha
muda.
“T-Marc
haina tena uhusiano wa aina yoyote, rasmi au kwa njia yoyote ile na
Njwete. T-Marc inaamini kuwa haki itatendeka katika shauri ambalo Njwete
anatuhumiwa.”
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: