NDEGE mpya moja kati ya mbili ya Shirika la Ndege (ATCL) kwa mara ya
kwanza imeruka, ikiwa ni sehemu ya kufanyiwa ukaguzi kabla ya kuanza
rasmi safari zake.
Ndege hiyo aina ya Bombardier Dash 8-Q400 iliruka saa 9:20 alasiri
kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar
es Salaam tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Kigoma na baadaye
Mwanza.
Marubani wa Kitanzania wakishirikiana na marubani wa kutoka Canada
waliokuja na ndege hiyo kwa mara ya kwanza, walirusha ndege hiyo ikiwa
ni hatua ya kufanyiwa ukaguzi na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA).
Akizungumza kabla ya kuruka na ndege hiyo, Meneja wa Kitengo cha
Dharura, John Chaggu alisema ndege hiyo inaruka kwa mara ya kwanza kwa
majaribio na kufanyiwa ukaguzi kabla ya kuruhusiwa rasmi na TCAA.
“Juzi tulifanyiwa ukaguzi wa kuangalia namna ya kuwahudumia abiria na
inapotokea dharura jinsi gani tutawahudumia na kuhakikisha wako salama,
hatua hiyo tumefaulu vizuri sana. Hii ya leo (jana) siyo ndege ya
kibiashara, hatutabeba abiria wa aina yeyote zaidi ya watu wachache
ambao wanahusika katika kufanya ukaguzi huu. Hii ya leo (jana)
tunakwenda Kigoma baada ya hapo Mwanza halafu tunarudi tena Dar es
Salaam,” alisema Chaggu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: