Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameziagiza
halmashauri nchini kuhakikisha zinaboresha miundombinu kwa wasioona,
ikiwamo kusimamia upatikanaji huduma za afya bure kama Serikali
ilivyoelekeza.
Pia,
ameishauri Serikali kupitia upya sheria na sera za upatikanaji huduma
muhimu kwa watu wenye ulemavu hususan matibabu na ajira serikalini na
taasisi binafsi.
Dk
Tulia amesema hayo wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya fimbo nyeupe kwa
watu wasioona yaliyofanyika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya na
kuhudhuriwa viongozi mbalimbali.
Amesema
kuelekea Tanzania ya viwanda, Serikali imeelekeza nguvu katika kutoa
ajira kwa walemavu ili kuwajengea mazingira mazuri ya kuishi na
kuanzisha shughuli za ujasiriamali, zitakazosaidia kujikwamua na
umaskini ili kuondokana na utegemezi.
“Viongozi
mmesikia wenzetu wanalalamikia huduma za afya, sasa ni wakati wa
kuhakikisha mnawasimamia vyema katika upatikanaji wa huduma za afya,
elimu bure na kusikiliza changamoto zinazowakabili,” amesema.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema mkoa una walemavu wasioona 603,
kati yao 223 ni wanaume na 380 wanawake na Serikali imeboresha
upatikanaji wa huduma za afya bure.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: