SERIKALI kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imesema kuwa
mkataba wa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kukodishwa klabu hiyo ni
batili. Tamko hilo limetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohamed
Kiganja baada ya juzi kusambaa kwa taarifa ya mkataba wa Yanga katika
mitandao ya kijamii.
Suala la Yanga kukodishwa timu lilianza mchakato tangu Manji aitishe
mkutano mkuu wa dharura miezi miwili iliyopita, akiomba ridhaa ya
wanachama wa klabu hiyo kumkodisha timu na nembo kwa miaka 10, ombi
ambalo lilipitishwa na kurudishwa katika bodi ya wadhamini kwa ajili ya
kufanyiwa kazi na juzi kupitishwa kwa makubaliano hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kiganja alisema wanaunga
mkono suala la mabadiliko, lakini lazima yafuate sheria na taratibu
zilizowekwa ili kukamilisha mabadiliko yoyote.
“Mimi sipingi klabu zetu kufanya mabadiliko isipokuwa najaribu
kukumbusha zifuate utaratibu wa kisheria, kwa sababu unapobadilisha jina
au kufanya marekebisho yoyote ni lazima vikasajiliwe na
kutambulika,”alisema.
Kiganja alisema hata Bodi ya Yanga iliyohusika kuruhusu timu hiyo
kukodishwa haitambuliki kwa Msajili, kwa vile wajumbe wake wengi ni wale
waliochaguliwa kwa mpito. Alisema bodi ya wadhamini iliyoundwa Julai 5,
1973 ni wawili tu wanaotambulika waliopo hadi sasa ambao ni Jabir
Katundu na Juma Mwambelo.
Lakini, Mwembelo amekuwa ahusishwi tena katika mambo yanayoendelea ya
timu hiyo. Bodi ya mpito, ambayo Kiganja alisema hawakusajiliwa wala
kupitishwa kwenye mkutano mkuu kutokana na taratibu ni George Mkuchika,
Fatuma Karume, Francis Kifukwe, Amri Ramadhan, Juma Kambi na Abeid
Mohamed.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: