Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo, Hamphrey Polepole amewapiga marufuku wajumbe wa mashina na
viongozi wengine wa CCM kujihusisha na uidhinishaji mauzo ya ardhi,
huku akiwataka wananchi kuwa makini na kufuata utaratibu wa kisheria
wakati wa ununuzi.
Polepole
alitoa onyo hilo jana wakati wa mkutano na wakazi wa King’azi Juu, Kata
ya Kwembe, baada ya kuelezwa kuwa wana matatizo mengi ya ardhi
yanayotokana na baadhi viongozi kuuza eneo kwa mtu zaidi ya mmoja.
Wananchi
hao walimweleza kuwa, udanganyifu unaofanyika unatokana na baadhi ya
viongozi wa serikali za mitaa na wajumbe wa mashina wa CCM kula njama na
wamiliki wa maeneo, kuuzia watu eneo moja zaidi ya mara moja.
Polepole
alisema CCM ipo kwenye harakati za kujijenga, hivyo lazima kumaliza
migogoro hiyo kama sehemu ya kujirekebisha. Mwenyekiti wa mtaa huo,
Seleman Bheho alisema mwaka 2014/15 alipoingia madarakani .ofisi yake
ilikuwa akipata kesi za za ardhi nane mpaka 10 kwa siku, lakini sasa
zimepungua hadi tatu kwa wiki.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: