MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema wakati umefika wa
Tanzania kujitegemea kiuchumi, na kwamba, nchi haiko tayari kupokea
misaada yenye masharti, ambayo hayaendani na mila na desturi zetu.
“Hatukubali kupokea misaada ambayo ina masharti magumu, tubadilike na
tuendelee kuijenga Tanzania yetu, twendeni kwa mtindo wa kuijenga
Tanzania yetu, tubane matumizi, tukusanye mapato,” alisema Makamu wa
Rais jana wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya wakazi wa Dodoma.
Makamu wa Rais alisema wakati umefika kwa Tanzania kujitegemea, japo
haijafika asilimia 100 ya kujitegemea angalau iko asilimia 60.
“Tunasema tunaendesha serikali hii kwa mapato yetu ya ndani. Mapato
ya nje tumetumia kwa miaka mingi nadhani sasa hivi wanaona Tanzania
tumetumia mapato yao muda mrefu kwa hiyo sasa wanakuja na kivuli cha
kutupa masharti, mengine yako magumu kwa mila na desturi zetu
hayatekelezeki na tunaposema hatutaki wanasema tunatoa fedha kwenye eneo
lile wanatutishia kwenye eneo la ARV kwani wanajua tukikataa ndugu zetu
watapukutika na wanaona tukiwabana hapa watakubali,” alisema.
“Tumeanza kurekebisha sheria ya manunuzi angalau sio njia hii wapita
njia ile ili wafanye manunuzi,” alisema Makamu wa Rais. Aliongeza kuwa
kuna mapungufu ya mapato kwenye halmashauri nchini kutokana na sababu za
kutokusanywa au zikikusanywa zinaliwa.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: