ads


dc-kongwa-444

Meneja wa Mamlaka ya Maji katika mji wa Kongwa mkoani Dodoma, Tshabonga  amesimamishwa kazi kutokana na kushindwa kusimamia upatikanaji wa maji.

Hatua hiyo, imechukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi aliyebainisha kwamba amemsimamisha meneja huyo na kumteua Mtaalamu wa Maji wa Wilaya, Hamisi Ally kushika nafasi hiyo kwa kuhakikisha maji yanapatikana kwa wingi.

Ndejembi alieleza kuwa katika uchunguzi wake amebaini kuwa mamlaka hiyo ya maji ina uongozi mbovu ambao hautekelezi wajibu wake na haujali shida za wananchi juu ya suala zima la maji.

Pia alieleza kwamba katika vipaumbele vyake katika Wilaya ya Kongwa, maji ni namba moja hivyo atahakikisha maji yanapatikana kwa wingi na kuweka kumbukumbu yake ya uongozi kwa wananchi wa Kongwa kwani wameteseka zaidi ya kipindi cha mwaka mzima.

Katika mwanzo wa operesheni yake ya kurudisha upatikanaji wa maji, Ndejembi alitembelea vichoteo vya maji vilivyopo katika vijiji vya Sogelea A na B Kata ya Sagara na kuwataka wale wote wanaofanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji wa mbogamboga kuacha mara moja ili maji yaweze kujaa kwenye matangi na kuwafikia wananchi.
dc-kongawa-3

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Yohana Muse alisema wamefarijika na kauli ya Mkuu wa Wilaya na kumuomba asimamie kurekebishwa ratiba za maji ili hata kama yatapatikana kwa uchache basi kila mtaa upate maji siku moja katika wiki.

Ndejembi amemaliza mgogoro wa ardhi uliokuwepo kwa muda mrefu kati ya Shule ya Msingi Mnyakongo na Kanisa Katoliki la Kongwa kwa kuwapatia kanisa eneo jingine kwa ajili ya kujenga shule binafsi ya bweni na Shule ya Mnyakongo kubaki na eneo lililokuwa likigombaniwa.

Ameahidi kujitahidi kamaliza migogoro ya ardhi iliyopo katika wilaya yake kwani inakwamisha shughuli nyingi za maendeleo kwa wananchi na kuahidi kuwabana viongozi wanaosababisha au kuchochea migogoro hiyo.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: