ads


kigwangalla

Mbali na tatizo la kiuchumi, utashi wa wanasiasa kutotilia mkazo asilimia moja ya Pato la Taifa kutumika kwenye tafiti na ubunifu ndio moja ya sababu ya kushindwa kuwaendeleza wanasayansi hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangala wakati wa kufunga mkutano wa siku tatu wa wanasayansi uliofanyika jijini Dar es Salaam, Alisema serikali inafahamu changamoto nyingi ambazo zinawakabili wanasayansi kama changamoto ya fedha, fursa za kujiendeleza, uchumi mdogo na utashi wa kisiasa.

Dk Kigwangala aliongeza kuwa, “pia tungeweza, kuwekeza fedha zetu kwenye kufanya tafiti, ambazo zinalenga kutatua matatizo yanayotusibu kila siku, kuliko tafiti ambazo zinatokana na fedha za wafadhili jambo ambazo masharti ni kufanya utafiti kulingana na malengo ya watoa fedha.”, Aidha alisema wataendelea kufanywa ushawishi ili itengwe bajeti ya kutosha, kwa ajili wanasayansi wa ndani ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanya tafiti na ubunifu kwani Tanzania ya kesho itategemea sayansi na ufumbuzi.

Dk Kigwangala alisema mapendekezo sita yaliyofikiwa kwenye mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), yatafanyiwa kazi kwa sababu serikali inaamini kwenye kupanga mipango na kutunga sera, ambazo zinatokana na ushahidi wa kiutafiti na mijadala ya kisayansi.

Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk Mwele Malecela alisema kongamano hilo lililoshirikisha washiriki 320, limekuja na mapendekezo kadhaa ambayo ni kuanzishwa kwa kituo cha kupambana na magonjwa ya virusi yanayoenezwa na mbu, kuimarisha maabara katika afya msingi, ikiwa ni njia ya kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza.

Alisema pia mkutano huo umependekeza umuhimu wa kuwapo juhudi za makusudi za kuongeza utafiti na uvumbuzi miongoni mwa watanzania, na pia kutolewa elimu sahihi ya namna ya kutuza, kuandaa mazao na chakula na namna ya kulisha.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: