ads

Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye kwa sasa anavizuri na wimbo wake 'Salome' amefunguka na kusema kuwa wimbo huo uliwavuruga wasanii wengi wakubwa duniani kabla hajatoka hata baada ya kutoka.


Diamond Ploatnumz alisema hayo kwenye Friday Night Live (FNL) na kudai kuwa wimbo huo yeye mwenyewe anashindwa kuelewa una nini kutokana na jinsi ambavyo umeweza kupokelewa vizuri na kupendwa na watu wengi sana duniani.

"Kiukweli kabisa hata wakati napata wazo kusema nifanye wimbo wa 'Salome' nilikuwa nasema ni wimbo fulani mzuri kiasi kwamba hata mtu asipoelewa lugha lakini anaweza kuipenda, nikumbuka hata wakati Mama yule Said Karoli alipoimba wimbo ule na ulipokuwa unavuma tulikuwa hatuelewi anazungumza nini lakini tuliipenda na ilikuwa nzuri na ilivuma sana, kwa hiyo nikasema kwa sasa hivi soko lilivyokuwa na nikiwatizama Watanzania nikichukua wimbo ule nikatia vitu vyangu fulani hivi itakuwa kali zaidi. Saizi wimbo huu Afrika na sehemu ambazo wanatutizama imekuwa kubwa nafikiri watakuwa wameipenda sana hata ukiangalia 'Comments' zao kwenye video ile 'Youtube' unaona kuwa wameipenda.

 Kabla ya wimbo kutoka Wizkid alikuwa Tanzania wakati nipo naye nilimpa ule wimbo aisee ulimvuruga sana, nilipata bahati ya kuwa na Mheshimu Rais Mstaafu Jakaya Kikwete naye aliupenda sana, hata baada ya wimbo kutoka wasanii wakubwa kama wakina Teckno, Flavour walinitumia ujumbe mfupi kuonyesha kupenda nakumbuka hata Neyo naye aliniambia 'I like the song'" alisema Diamond Platnumz

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: