Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amekutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya CRCC ya China,
Fengchao Meng ambaye amemuahidi kushiriana na Serikali kuboresha
miundombinu ya Mkoa wa Dodoma.
Mwenyekiti
huo ameongozana na Mwenyekiti wa Kampuni nyingine ya Ujenzi ya CCECC ya
China, Yuan Li na Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki kati ya Serikali za
Tanzania na China, Joseph Kahama.
Majaliwa amesema kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni uendelezaji wa Dodoma.
Amesema
nchi hizo ni marafiki wa muda mrefu ambazo zinashirikiana vizuri
katika ujenzi wa miundombinu, hivyo Serikali inatarajia mengi kutoka
kwenye kampuni hiyo.
“Dodoma
kuna fursa za uwekezaji kwenye sekta nyingi kama miundombinu, kilimo na
viwanda. Mnaweza kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za makazi, ofisi,
huduma za jamii na viwanda,” alisema.
Meng
amesema kampuni yake itaungana na Serikali kuboresha Dodoma,
inatarajia kutuma wataalamu wake mkoani humo kuangalia maeneo ya
uwekezaji.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: