ads

CHAMA cha ACT Wazalendo kimejibu mapigo ya kauli zilizotolewa na Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christopher ole Sendeka, huku kikieleza kuwa kinakaribisha uchunguzi juu ya mali na madeni za Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto.


Aidha, chama hicho kimeeleza kuwa kitafurahishwa zaidi kama uchunguzi huo, utahusisha akaunti zake za benki na mfumo wa maisha yake binafsi.

Tamko hilo lilitolewa na Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa wa chama hicho, Habibu Mchange wakati akizungumza na wanahabari katika Makao Makuu ya ofisi za chama hicho zilizopo Kijitonyama Dar es Salaam jana. Mchange alisema wameshtushwa na kusikitishwa na tuhuma zilizotolewa na Sendeka ambazo hazina ukweli wowote.

“Tunavitaka vyombo vya uchunguzi vianze kazi hiyo mara moja, kwani tunaamini kuwa kama kuna kiongozi ambaye mali, madeni, maslahi na akaunti zake ziko wazi basi ni ndugu Zitto,” alisema Mchange.

Alisema kuwa Katiba na Kanuni za chama hicho huwataka viongozi wote wa chama kuweka hadharani tamko la mali zao na madeni, na kwamba Zitto alitekeleza matakwa hayo ya kisheria na mali pamoja na madeni yake yako hadharani katika mitandao ya kijamii.

Akizungumzia kuhusu Sendeka kutaka uchunguzi dhidi ya wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge ambao walikuwa wakisimamia mashirika ambayo yanatajwa kufanya vibaya ikiwemo Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF na kumtaja Zitto, Mchange alisema, Sendeka pamoja chama chake ni kama wanaweweseka.

Alisema chama hicho kina taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambayo alitoa hati safi kwa Shirika la NSSF kwa hesabu za mwaka 2014/2015, ambayo ilimaanisha hakuona ufisadi wa aina yoyote.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: