SERIKALI imekubali kununua asilimia nane ya hisa za kiwanda cha
kusafishia mafuta, kitakachojengwa Uganda kwa Dola za Marekani milioni
150, sawa na karibu Sh trilioni tatu. Aidha, inaangalia endapo fedha
hizo zitatoka serikalini moja kwa moja au katika sekta binafsi au kwa
kushirikiana na sekta hizo ili kununua hisa hizo.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo, baada ya kufungua kikao cha kwanza cha majadiliano ya
utekelezaji wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanga,
kilichofanyika Dar es Salaam.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Waziri wa Maendeleo ya Nishati
na Madini wa Uganda, Irene Muloni, Profesa Muhongo alisema, asilimia 40
ya hisa za kiwanda hicho zitauzwa kwa nchi tano wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki, ambapo kila nchi itanunua asilimia nane ya hisa za
kampuni hizo.
Alisema ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu Dola za Marekani bil 4.7.
Akizungumzia kikao chao, Profesa Muhongo alisema, kilihusisha wataalamu
mbalimbali wa nchi hizo mbili ili kuangalia jinsi utekelezaji wa ujenzi
wa bomba hilo utakavyofanyika.
“Nimepewa maagizo na Rais, lakini pia mwenzangu amepewa maagizo na
Rais wa Uganda kwamba hii kazi ianze haraka na ikiwezekana ikamilike
kabla ya wakati uliopangwa,” alisema Profesa Muhongo
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: