KOCHA wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, Hans Pluijm ametamba
timu yake leo kuibuka na ushindi dhidi ya Toto Africans ili kuzidi
kukaribia kutetea taji hilo.
Akizungumza wakati wa mazoezi ya timu hiyo
jijini hapa, Pluijm alisema kuwa licha ya uzuri wa Toto Africans, lakini
wataibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo CCM Kirumba.
Alisema wachezaji wake mwanzo mwisho watacheza kwa kujituma huku
wakilishambulia kwa nguvu lango la Toto African wakisaka pointi tatu
muhimu. “Toto African ni timu iliyojaa wachezaji wadogo wanaojituma na
wanacheza mpira mzuri sana.
Jambo muhimu kwetu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi ili tuweze
kubaki kileleni mwa Ligi Kuu na kutwaa taji,“ alisema Pluijm. Hata
hivyo, Pluijm alithibitisha kikosi chake kuwa na majeruhi, lakini
amesema wameziba mapengo hayo.
“Golikipa wetu Barthez na Godfrey Mwashiuya ni majeruhi ila nina
imani mapengo yao yatazibwa na wachezaji waliopo,” alisema Pluijm. Kwa
upande wake kocha mkuu wa Toto Africans, Dominik Glawogger alisema
anategemea vijana wake watacheza vyema na kuweza kuifunga Yanga.
“Baada ya mchezo na Simba tuliwapa wachezaji wetu mapumziko ya siku
tatu kutokana na mechi ngumu tuliyokuwa nayo, lakini sasa walirudi
wachezaji na tangu Jumatatu tulianza mazoezi na Jumamosi (leo)
tunategemea kushinda,” alisema Dominik.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: