WAKATI keshokutwa ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani,
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema
utafiti uliofanywa hivi karibuni na waandishi wa habari wasio na mipaka
katika nchi 180, umebaini kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika
Mashariki kwa kutunza uhuru wa vyombo vya habari.
Akizungumza bungeni jana, Nape alisema kimataifa, Tanzania imeshika
nafasi ya 71 na hivyo kuwa moja ya mataifa yanayofanya vizuri duniani
katika kutunza uhuru wa vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa Nape, utafiti huo ni uthibitisho dhahiri kuwa madai
yanayoibuliwa na baadhi ya wabunge na wadau wengine kwamba Serikali
inaminya uhuru huo, si ya kweli.
“Tanzania tunafanya vizuri kimataifa na
hata kwa nchi za Afrika Mashariki tumekuwa wa kwanza kwa kuhifadhi
uhuru huo, hili linafuta dhana inayojaribu kujengwa ya kwamba uhuru
unaminywa, hii ni taarifa ya kitafiti na si suala la kubuni,” alisema
Nape.
Alisema dhana inayojengwa na baadhi ya wabunge kuwa kuna mwingiliano
mkubwa kati ya Serikali na Bunge, baadhi ya wabunge kusema studio ya
Bunge inaendeshwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), ni madai ya
uongo.
Alifafanua kuwa studio hiyo ya Bunge inaendeshwa na Bunge na
kilichofanyika ni kuomba msaada wa kitaalamu kutoka TBC, ili kusaidia
studio hiyo hadi hapo Bunge litakapopata wataalamu wake.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: