SIKU chache baada ya Rais John Magufuli kutaja idadi ya watumishi
hewa kuwa ni 7,200, msako unaoendelea katika utumishi wa umma, umetoa
takwimu mpya ambapo sasa watumishi hao wamefikia 8,236.
Katika hatua nyingine, wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ambao
wamefunguliwa kesi mahakamani kutokana na ubadhirifu, ambao wamekuwa
wanatumia magari na mafuta ya umma na kujilipa posho wanapokwenda kwenye
kesi zao, wataanza kuchukuliwa hatua kali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Angela Kairuki, amesema hayo bungeni jana wakati
akihitimisha hotuba yake ya bajeti kwa mwaka ujao wa fedha.
Akizungumzia wafanyakazi hewa, Waziri Kairuki alisema kati ya Machi
Mosi na Aprili 24, mwaka huu, Serikali imebaini kuwepo kwa watumishi
hewa 8,236, idadi inayoonesha kuwepo kwa ongezeko kubwa baada ya hivi
karibuni Rais kuripoti kuwepo wafanyakazi hewa 7,200.
Alisema katika idadi hiyo, wafanyakazi hewa 1,614 wameripotiwa kutoka
Serikali Kuu huku wengine 6,622 wakiripotiwa kutoka Serikali za Mitaa,
na kufanya ongezeko lao kufikia 2,737.
Kwa mujibu wa Waziri Kairuki, kuwepo kwa wafanyakazi hao hewa katika
utumishi wa umma kumeisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 15.4,
ambazo zingeweza kutumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: