KINARA wa mabao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, Amissi Tambwe, amesema
viwanja vya mikoani vitampa taji la mfungaji bora msimu huu na
atafikisha mabao 25.
Yanga imebakisha mechi tatu kumaliza ligi na zote itacheza ugenini
katika viwanja vya Nangwanda Sijaona, Mtwara, Sokoine, Mbeya na Majimaji
Songea.
Tambwe amesema katika mechi hizo ana uhakika wa kufunga mabao matano na kufikisha mabao 25 na kubeba tuzo hiyo ya mfungaji bora.
Tambwe ambaye sasa ana mabao 20, alisema
pamoja na ubovu wa viwanja vya mikoani, lakini yeye amekuwa akivijulia
na kufunga mabao muhimu kwa timu yake, ambayo kwa sasa ipo nafasi nzuri
ya kunyakua ubingwa msimu huu.
“Nina uzoefu mkubwa na viwanja vya mikoani kwa sababu uwanja
ninaofanya mazoezi yangu binafsi ni mbaya kama vilivyo vya mikoani,
ndiyo maana mimi huwa ninapocheza huko nafanya vizuri,” alisema Tambwe.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: