Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa
mara nyingine amelazimika kuzungumza na wananchi wa Arusha Mjini
waliokuwa wamezuia msafara wake uliokuwa ukitoka Chuo cha Mafunzo ya
Kijeshi Monduli kwenda Ikulu ndogo ya Arusha.
Rais Magufuli amerejea kauli yake kuwa serikali yake haitawavumilia
viongozi na watumishi wa umma ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo
vya rushwa na ufisadi, huku akisema ataendelea kutumbua majipu kwa
yeyote atakayebainika kuchezea mali za umma ili kulinda maslai ya wengi,
hususani watanzania wanyonge.
"Ninafanya kwa niaba yenu, ninafanya kwa niaba yenu, ningekuwa
sifanyi kwa niaba yenu, na mimi ningeingia madarakani ningeanza
kushirikiana na hao, na wengine walifikiria nitashirikiana nao,
wamekwama mimi nitawatumbua kila siku ili Tanzania iwe ya neema iweze
kwenda mbele, haiwezekani nchi kama hii tajiri, Tanzanite ipo, dhahabu
ipo, wanyama mpaka nyani wameanza kuuzwa, wakimalizika nyani si tutauzwa
na sisi ndugu zangu, ni lazima nisimamie hili" amesisitiza Dkt.
Magufuli.
Aidha katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amewahakikishia kuwa
serikali yake imeanza kuwashughulikia wafanyabiashara ambao wameficha
sukari kwa makusudi na kusababisha upungufu wa bidhaa hiyo.
Rais Magufuli amesema tayari vyombo vya dola vimekamata tani 5,000 za
sukari iliyofichwa na mfanyabiashara mmoja huko Tabata Jijini Dar es
salaam na pia vimembaini mfanyabiashara mwingine aliyeficha sukari hiyo
Jijini Arusha.
"Kweli nitawakomesha hawa, wasije wakanilaumu, haiwezekani ukaficha
sukari wakati viwanda vyetu vinatengeneza sukari, kuna mmoja mwingine
yupo Arusha hapa, nae ameficha sukari, alienda akanunua kwenye viwanda
vya sukari vya hapa akaificha yote, leo ninamshughulikia.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: