ads

SALMA Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ameonesha kukerwa na wale wanaoshambulia utawala wa mumewe (Rais Kikwete). 


 Mama Salma amesema hayo  kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake (UWT) unaofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao Makuu.

“Kila mwaka naendelea kuisemea serikali iliyopo madarakani mambo mazuri, acheni hali ya kukaa na kuanza kusema kwamba serikali ile ilikuwa vile na serikali hii iko hivi.

“Wala msisema yule alikuwa vile na huyu yuko hivi, kwa kumalizia hayo napenda kusema mume wangu ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa anawasalimia sana,” amesema Mama Salma.

Akizungumzia utumbuaji wa majipu amesema, serikali kwa sasa imeanza kutumbua majipu makubwa kuanzia juu lakini zipo taarifa kuwa, yapo majipu mengine ngazi za chini pia ndani ya CCM.


Amesema, “kila anayejitambua kuwa ni jipu kabla hajafikiwa ni bora akajitumbua mwenyewe au ajipake spriti ili jipu hilo lipoke mapema kabla halijatumbuliwa.”

Hata hivyo ameonesha wasiwasi kuwa, kuna uwezekano miradi mingi ya UWT ikachukuliwa kutokana na umoja huo kuwa na mali ambazo zinaonekana kumilikiwa bila kufuata taratibu.

Amesema, kwa upande wa ardhi kuna viwanja vingi ambavyo havina hati na vimekaa muda mrefu bila kuendelezwa jambo ambalo kwa sasa mameya wanaweza kuvibadilishia matumizi.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: