MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Ismail Rage, amezidi kuwabana viongozi
wa Simba na kusema hawapaswi kuendelea kunyamaza kuhusiana na fedha za
mauzo ya mshambuliaji Emmanuel Okwi badala yake waweke wazi.
Rage alisema kuwa fedha hizo pamoja na za
mshambuliaji Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji zina uwezo
wa kujenga uwanja wa Bunju, kuweka nyasi na majukwaa, lakini ukimya wa
viongozi wa Simba kuhusu jambo hilo unamtisha.
“Nimeamua kuzikomalia kwa vile nilishutumiwa sana wakati wa uongozi
wangu kuwa nilikula zile fedha. Lakini nashukuru fedha zimeletwa na
waliokuwa wananituhumu baadhi yao ndiyo hao wameamua kunyamaza.
“Wawaeleze wanachama matumizi ya hizo fedha, zile za Okwi zishaletwa
zaidi ya Sh milioni 600, halafu za mgawo wa mauzo ya Samata kutoka TP
Mazembe kwenda Ubelgiji nazo zipo njiani,” alisema Rage.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: