Serikali imesema kwamba haitawalipa watu wote ambao wamebomolewa nyumba
zao kwa kujenga mabondeni au kujenga maeneo ya wazi,hifadhi ya barabara,
au maeneo yaliyotengwa kwa shughuli maalumu.
Hayo yameelezwa Bungeni na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Bi. Angelina Mabula wakati akijibu swali la Mbunge wa Wingwi
Kisiwani Zanzibar Juma Kombo Hamad ambaye ametaka kujua ni lini serikali
itawalipa fidia wananchi ambao wamevunjiwa nyumba zao bila ya serikali
kuwalipa kwani wakati wakijenga serikali iliwaona na kukaa kimnya.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Mabul amesema kwamba kwa mujibu wa
sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na sheria ya mipango miji ya mwaka
2007 inaweka bayana sehemu ambazo wananchi hawatakiwi kujenga ikiwemo
maeneo oevu, mabondeni, na vyanzo vya maji ambapo mwananchi akitaka
kujenga ni lazima ajenge umbali wa mita 60 maeneo hayo.
Bi. Mabula ameongeza kuwa kutokana na wananchi kukiuka maagizo hayo
serikali haitawalipa fidia hivyo ni wajibu wa wananchi kufuata sheria za
nchi ili kuepuka migongano isiyo ya lazima.
Aidha Bi. Mabula amezitaka halmashauri kote nchini kuwa makini katika
kusimamia sheria kwani imebainika kwamba nyumba nyingi huwekwa X na
halmashauri lakini ufuatiliaji unakuwa haupo ndiyo maana matatizo hayo
yamekuwa yakijirudia
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: