MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema jukumu kubwa la nchi za
ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika ni kuhakikisha zinaweka
mazingira mazuri ya kuwezesha wanawake kiuchumi.
Samia aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye ufunguzi wa mkutano
kuhusu masuala ya kuwezesha wanawake kiuchumi kwa nchi za Mashariki na
Kusini mwa Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo uliandaliwa na Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliloliteua mwanzoni mwa mwaka huu kwa
ajili ya kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya
kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi kupitia utekelezaji wa
Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu.
Jopo hilo lenye viongozi na wataalamu mbalimbali, Samia akiwa
miongoni wa wajumbe wa jopo hilo, limezinduliwa Machi 15, mwaka huu
sambamba na mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya
Wanawake.
Makamu wa Rais alisema pamoja na kuwepo kwa jitihada mbalimbali za
kuinua wanawake kiuchumi bado mazingira hayampi nafasi na hasa kwa
wanawake wa ngazi za chini, wengi wao wakiishi vijijini kutokana na
changamoto zinazokwamisha jitihada hizo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: