SERIKALI ya Awamu ya Tano imeanza kutekeleza kwa vitendo azma yake ya
kujenga uchumi unaotegemea viwanda baada ya kuzindua ujenzi wa mradi
maalumu wa uwekezaji wa viwanda mkoani Morogoro ili kukuza uchumi na
kuongeza ajira nyingi kwa vijana nchini.
Utekelezaji huo ni kutokana na Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Charles Mwijage juzi kuzindua eneo maalumu la ujenzi wa miradi
ya uwekezaji la Star City katika Manispaa ya Morogoro.
Eneo hilo la miradi ya uwekezaji lina ukubwa wa ekari 10,661 na
lilikuwa ni shamba la mkonge Tungi Sisal Estate ambalo kwa sasa
likijulikana kwa jina la Dominio Plantation Limited (DPL).
Waziri Mwijage kabla ya kuzindua eneo hilo maalumu la uwekezaji,
alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli imeanza
utekelezaji wa Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kuanza na Mkoa wa
Morogoro.
“Morogoro haijapendelewa isipokuwa ina historia tangu wakati wa
Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambapo
Waziri Jamal (Amir) aliwezesha kujengwa kwa viwanda hivi hapa Morogoro,”
alieleza Mwijage na kuongeza: “Morogoro ina bahati ya kuwa na sifa ya
kujenga viwanda kutokana na mazingira na jiografia yake naweza kusema
ina bahati ya kuzaliwa ilivyoumbwa na Mungu kuvutia uwekezaji.”
Alisema ujenzi wa viwanda katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa ya
uwekezaji ni mpango wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kuona vinawatoa
vijana kwenye kucheza ‘pool’, bao na kukaa vijiweni ili wajikite katika
shughuli halali za uzalishaji mali viwandani ili kujipatia kipato na
kukuza uchumi wa taifa.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: