ads
Wakuu wa Idara zote za jiji la dsm pamoja na maafisa Utumishi wa halmashauri za jiji wamesaini kiapo cha kazi mbele ya Mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya baada ya kubainika kutoa taarifa zisizo za kweli dhidi ya kuwepo kwa watumishi hewa katika idara zao baada ya kubainika watumishi hewa wengine 209 katika Uchunguzi wa Siku chache zilizopita.

Miongoni mwa masharti yaliokuwapo katika kiapo hicho ni kwamba iwapo ikigundulika kuwapo kwa watumishi hewa katika idara husika baada wiki moja ijayo,Afisa utumishi au mkuu wa idara hiyo atalipa gharama za mishahara iliyopotea,kushitakiwa kwa uhujumu uchumi,kuachishwa kazi lakini pia kufikishwa mahakamani.
Hatua ya kusaini na kula kiapo inatokana na baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa Utumishi katika jiji la DSM kudaiwa kutoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa mkoa Paul Makonda na wakuu wa wilaya za jiji hilo baada ya kutoa idadi ndogo ya watumishi hewa kwa mkoa wa dsm ambao walikuwa 74 tu, huku uhakiki wa sasa uliofanywa na tume maalum ukibaini watumishi hewa 209 ambao wametafuna kiasi cha takribani shilingi bilion 2.7
Kiapo hicho cha kazi kiliionekana kuwa mwiba kwa watumishi hao wa mkoa wa DSM kutokana na wengi wao kushindwa kujaza,huku wakileta hoja ambazo zilionekana kutokuwa na nguvu kwa mkuu wa mkoa kwa kuogopa kujifunga mpaka pale Bwana Makonda alipotoa dakika 5 kujaza na kuwasilisha.
Baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa utumishi wamesema kiapo hicho ni kizuri kwa ajili ya Utendaji kazi lakini ni mwiba kwa wakuu wa idara hasa kutokana na wengi wao kufanya kazi kwa mazoea, huku Katibu tawala wa mkoa wa Dsm THERESIA MBANDO akikiri kuwepo kwa taarifa zenye utata juu ya idadi ya watumishi hewa.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: