WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, amesema Serikali ya
Awamu ya Nne iliyokuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete haikukomba fedha
katika Hazina kama ambavyo baadhi ya wabunge wamedai, hata Shirika la
Kimataifa la Fedha (IMF), lilifanya tathmini na kutoa taarifa safi.
Dk Mpango alieleza hayo bungeni jana mjini hapa, wakati akijibu hoja
mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia mjadala wa wizara
mbili zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Utawala Bora, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma.
Katika mjadala huo, baadhi ya wabunge walisema Serikali ya Awamu ya
Nne, ilikomba fedha zote Hazina na kusababisha Serikali ya Awamu ya Tano
chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, kukuta Hazina haina fedha.
Akijibu hoja hiyo, alisema hakuna ushahidi ulioitia hatiani Serikali
ya Awamu wa Nne kuhusu kukomba fedha Hazina na kwamba IMF na wadau
wengine wa kimataifa, walifanya tathmini huru ya bajeti na mwenendo wa
uchumi nchini na taarifa yao ya mwisho waliitoa Desemba mwaka 2015.
Katika ripoti hiyo hakuna mahali ilipoonesha nchi ilikuwa na hali
mbaya ya fedha na kwamba kwa kudhihirisha hilo, vigezo vya kimataifa
vilionesha bayana kuwa Deni la Taifa ni himilivu na nchi bado
inakopesheka na imeendelea kulipa mishahara watumishi wake pamoja na
madeni mengine bila kutetereka.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: