Katika kukabiliana na upungufu wa uzalishaji wa umeme wa kutosha
Serikali imefanya mapitio ya ripoti ya kuendeleza nishati ya joto ardhi
kwa lengo la kuongeza uzalishaji mwingine wa umeme ambao utasaidia kwa
watanzania kupata dira ya maendeleo na kuongeza maendeleo ya uchumi wa
Taifa .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam kwa niaba ya
waziri wa nishati Madini, Prof Sospeter Muhongo Naibu katibu mkuu
Wizara ya Nishati na Madini DK. Mhandisi JULIANA PALLANGYO amesema
kuwa kuanzisha kwa umeme wa jotoardhi unaotokana na mwamba wenye joto
unaochemsha maji yaliyoingia ardhini ambapo utasaidia kupunguza kwa
kiasi kikubwa uhaba wa umeme hapa inchini .
Aidha maeneo yaliyolengwa ni Manyara ,ngozi ngorongoro ,kisaki
majimoto mara na mengineyo ambapo mvuke wake ni msafi hauna madhara
yeyote ambao huweza kutumika kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani
,viwandani kilimo na dawa .
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kuendeleza Jotoardhi
Tanzania (TGDC) Eng Boniface Njombe amesema kuwa ilianzishwa Desembar
2013 kwa madhumuni ya kusimamia na kuongeza maendeleo ya ya jotoardhi
nchini ambapo kuzalisha megawaiti 200 ifikapo mwaka 2020 na mega waiti
500 ifikapo mwaka 2025.na 2033 itazalisha megaweti 800 .
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: