Mshambuliaji wa kimataifa Thomas Emmanuel Ulimwengu amesema kwamba kwa
sasa pengo la Mtanzania mwenzake, Mbwana Ally Samatta linaonekana TP
Mazembe.
Ulimwengu alisema TP Mazembe kwa sasa inamkosa mjanja na mwepesi, mwenye uwezo wa kufunga kama Samatta.
Samatta aliondoka timu hiyo ya DRC Januari mwaka huu baada ya kushinda nayo taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji anakoendelea vizuri hivi sasa.
Na tangu kuondoka kwa Samatta aliyekuwa kinara wa mabao wa timu hiyo ya Lubumbashi, Mazembe imeonekana kupoteza makali yake kiasi cha kuvuliwa mapema ubingwa wa Afrika.
Mazembe ilitolewa na Wydad Casablanca ya Morocco katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Katika mechi iliyopita Mazembe ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya Stade Gabesien Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi.
Ulimwengu aliyecheza kwa dakika 45 juzi kabla ya kutoka uwanjani akiwa anachechemea, alisema timu kwa sasa haina mtaalamu wa kufunga mabao kama alivyokuwa Samatta.
“Pengo la Samatta linaanza kuonekana sasa, pale mbele hakuna na anayeweza kufunga kama Samatta, tunapoteza nafasi nyingi sana, hilo ndilo tatizo,”amesema Ulimwengu.
Sasa Mazembe itakuwa na kibarua kigumu katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, ikitakiwa kwenda kuulinda ushindi huo mwembamba nchini Tunisia

DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: