RAIS John Magufuli amesisitiza kwamba kamwe hatakubaliana na
wafanyabiashara wachache wanaotaka kuwaumiza Watanzania na kuitakia
mabaya nchi, na atawashughulikia bila kujali vyama vyao.
Alisema kuna kikundi cha wafanyabiashara wachache sana kila kitu
wanataka wafanye wao bila hata kuwahurumia Watanzania na wanataka
kuiendesha nchi wanavyotaka ikiwa ni pamoja na kuingiza bidhaa wakati
wowote wanavyotaka na kuwaumiza Watanzania, hilo halitakubalika kamwe.
“Hapa kwangu ni mkong’oto tu. Kwa wale wafanyabiashara wenye kuitakia
mabaya nchi hilo halitavumiliwa… awe CCM, CHADEMA au CUF
atashughulikiwa kikamilifu,” alisema Rais Magufuli
“Hapa ni Tanzania kwanza na kuwajali wanyonge na mimi ni Rais wa
Watanzania na wala sibagui mtu.” Rais Magufuli alitumia nafasi hiyo
kuwaambia wakazi wa Arusha na vitongoji vyake kuwa uchaguzi umeshakwisha
na kinachotakiwa kwa sasa ni maendeleo kwa wote bila ya kujali chama,
dini wala kabila.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: