KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja amesema pamoja na kupoteza matumaini
ya ubingwa, lakini watajitahidi kuweka heshima kwa kushinda mechi zote
zilizosalia.
Simba ilizidi kupoteza mwelekeo wa kutwaa ubingwa baada ya kutoka
sare ya bila kufungana dhidi ya Azam katika mechi iliyochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Sare hiyo imefanya Simba kubaki nafasi ya tatu ikiwa na pointi 58,
huku Azam ikiwa ya pili na pointi 59 nyuma ya Yanga inayoongoza ligi
hiyo.
Akizungumza jana, Mayanja alikiri kupoteza mwelekeo baada ya sare na
Azam, lakini anaamini ushindi wa mechi zilizosalia utaipa timu yake
heshima.
“Ni kweli kabisa ile sare yetu na Azam iliharibu hesabu zetu, lakini
huo ndio mpira wa miguu ulivyo, kila timu inahitaji ushindi kwa mechi za
sasa… tunajipanga kushinda mechi zetu zote zilizosalia,” alisema.
Simba inatarajiwa kucheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki, mechi ambayo itakuwa ya vuta nikuvute kutokana
na timu hiyo kusheheni wachezaji wengi wazoefu waliopita timu
mbalimbali za Ligi Kuu ikiwemo Simba.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: