RIPOTI ya Prof. Mussa Juma Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imebaini taasisi 13 za serikali zilizofanya matumizi nje ya bajeti iliyopangwa .
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, taasisi hizo zimefanya matumizi nje ya bajeti na kugharimu Sh. 1,298,373,921 katika ukaguzi wa hesabu za mwaka 2014/15.
Taasisi hizo ni balozi tisa, wizara mbili na sekretarieti mbili za mikoa ambazo zimelipa kiasi hicho cha fedha kwa matumizi mbalimbali nje ya bajeti iliyoidhinishwa bila kutafuta idhini au kibali kinyume na Kanuni 46 (3) ya Kanuni za Fedha za Umma ya Mwaka 2001 (Iliyorejewa 2004).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya shughuli zilizopangwa hazikuweza kutekelezwa kama ilivyoidhinishwa kwenye bajeti.
Ripoti hiyo ya imebainisha kwamba Jumla ya matumizi hayo, kiasi cha Shilingi 147,662,326 kilikuwa matumizi nje ya bajeti na Shilingi 1,150,711,595 kilikuwa ni matumizi zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa.
Taasisi hizo 13 zilizofanya malipo nje ya matumizi ya bajeti na kiasi chake kwenye mabano ni ubalozi wa Tanzania Pretoria, Afrika Kusini ilikuwa (Sh. 27,813,874),Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Sh. 5,000,000).
Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia (Sh. 103,494,252), Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga (11,354,200), Ubalozi wa Tanzania, Pretoria, Afrika ya Kusini (Sh. 200,726,900), Ubalozi wa Tanzania-Maputo, Msumbiji (Sh. 146,847,102), Ubalozi wa Tanzania-Moroni, Comoro (Shilingi 374,890,135).
Nyingine ni Ofisi ya Waziri Mkuu (Shilingi 15,165,515), Ubalozi wa Tanzania- Lilongwe (Sh. 42,902,594), Ubalozi wa Tanzania-Beijing, China (Sh. 109,448,872), Ubalozi wa Tanzania-Moscow, Urusi (Shilingi 97,557,289), Ubalozi wa Tanzania-Rome, Italia (Sh.154,733,188), Sekretarieti ya Mkoa –Lindi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: