MAWAZIRI wa Serikali ya Awamu ya Tano wamewajia juu wabunge wa
upinzani na wananchi wanaovishutumu kila mara vyombo vya ulinzi nchini
na kuwataka kuacha kuvihusisha vyombo hivyo na masuala ya kisiasa.
Mawaziri hao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk
Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf
Masauni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira, January Makamba.
Wamewataka wananchi na hususani wabunge wa vyama vya upinzani,
kutambua kuwa vyombo hivyo vya ulinzi ambavyo ni pamoja na Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi wajibu wake mkubwa ni
kulinda mipaka ya nchi na usalama wa raia na mali zao.
Akizungumza wakati wa mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara inayoshughulikia Muungano na Mazingira, Dk Mwinyi
alisema haijawahi kutokea na wala haitotokea jeshi kutumika kisiasa.
Alisema Jeshi la Tanzania limekuwa likitekeleza majukumu yake kwa
kufuata sheria iliyojiwekea pamoja na za kimataifa na wala hata siku
moja haliwezi kutumika kwa ajili ya kutumiza malengo ya kundi fulani.
“Jeshi letu lina sifa ya kimataifa ya ulinzi wa amani, dunia kote
tunasifika kwa weledi, kulinda amani na mipaka yetu. Haijawahi kutokea
wala haitotokea jeshi kujiingiza kwenye shughuli za kisiasa,”
alisisitiza Dk Mwinyi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: