SERIKALI imesema vigogo wa juu katika utumishi wa umma,
watakaobainika kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha
ulipaji wa mishahara hewa, watafunguliwa kesi ya jinai.
Aidha, imesema ifikapo Julai mosi, mwaka huu Halmashauri zote nchini
ziwe zimefunga na kutumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya
mapato yake ya ndani na zimetakiwa kusitisha ukusanyaji kwa njia ya
mawakala.
Katika hatua nyingine imesema hadi kufikia Machi, 2016, watumishi 90
wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na wengine kufikishwa
mahakamani kwa kukiuka taratibu na sheria za kazi wakiwemo wakurugenzi
watendaji (DED) wa halmashauri watano ambao wamevuliwa madaraka.
Hayo yalisemwa kwa wakati tofauti na mawaziri wawili katika Ofisi ya
Rais, walipowasilisha hotuba za bajeti kwa ofisi zao kwa mwaka ujao wa
fedha bungeni mjini hapa jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi
na Utawala Bora, Angela Kairuki akiwasilisha hotuba ya ofisi hiyo,
alisema kuanzia sasa kiongozi wa serikali wakiwemo wa ngazi za juu
watakaobainika kuhusika kwa njia moja au nyingine katika kufanikisha
ulipaji wa mishahara hewa watafunguliwa kesi za jinai.
Waziri huyo alisema uchumi imara na endelevu katika nchi yoyote
unahitaji uwepo wa utumishi wa umma uliotukuka unaozingatia utawala
bora, utawala wa sheria, maadili na mifumo thabiti ya usimamizi na
utekelezaji.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: