KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja amesema beki Abdi Banda, bado anayo
nafasi ya kuitumikia timu hiyo endapo atarudi na kuwaomba msamaha
viongozi, wachezaji wenzake na mashabiki.
Banda hayupo kwenye kikosi cha Simba kwa muda mrefu, tangu
alipokorofishana na kocha huyo baada ya kugoma kupasha misuli ili aweze
kuingia uwanjani katika mchezo wa Coastal Union na Simba uliofanyika
Uwanja wa Mkwakwani Tanga katika Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea.
Mayanja alisema Banda alijifukuza
mwenyewe kwenye kikosi cha Simba tangu matatizo hayo yalipotokea mwezi
mmoja uliopita na yeye hakumfukuza, wala kuzungumza naye jambo lolote.
“Sijagombana na Banda, wala kumfukuza kwenye timu, isipokuwa yeye
mwenyewe ndio amejiondoka, lakini endapo atarudi na kuomba msamaha kwa
viongozi wetu, wachezaji wenzake na mashabiki atarudishwa kundini kwa
sababu ana mchango wake kwenye timu,”alisema Mayanja.
Kocha huyo alisema siku zote amekuwa akisimamia nidhamu kwa lengo la
kutaka vijana hao wafike mbali katika mchezo huo wa soka, lakini
anashangaa licha ya vipaji walivyokuwa navyo wamekuwa na kiburi ambacho
anaamini itakuwa ni kikwazo kikubwa cha kuwafanya washindwe kupata
mafanikio kupitia mchezo huo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: