WAKATI Yanga na Azam `zikilia’ kulundikiwa mechi mfululizo licha ya
kuwa na majukumu ya kimataifa, Kocha wa timu ya soka ya Simba, Jakson
Mayanja amesema ratiba mpya ni nzuri kwa klabu hizo, kwani itazisaidia
kujiimarisha na kufanya vizuri michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na
ile ya Kombe la Shirikisho.
Yanga inaisubiri Al Ahly katika mchezo utakaochezwa Aprili 9, mwaka
huu na Azam FC inawasubiri Esperance ya Tunisia katika mchezo
utakaochezwa siku moja baadaye. Hata hivyo, kabla ya kucheza michezo ya
kimataifa, Yanga na Azam kila moja itatakiwa kucheza michezo mitatu
ambayo kati ya hiyo, miwili ya ligi na mmoja wa Kombe la FA.
Kutokana na ratiba kubana viongozi wa Yanga na Azam waliiomba Bodi ya
Ligi Kuu Tanzania iwalegeze na kupunguza mechi ili kupata muda wa
maandalizi, lakini bado hawakukubaliwa. Lakini mtazamo wa `kubanwa’ wa
wawakilishi hao wa Tanzania, Mayanja amekuwa na mtazamo tofauti, akisema
ni vyema timu hizo zikacheza michezo hiyo kwani wachezaji wataendelea
kuimarika na kuwa na nguvu.
“Wao wanalalamikia ratiba imewabana badala wafurahi kuwa itawasaidia
kuwaimarisha wachezaji kuelekea michezo yao ya kimataifa, ni bora
waendelee kucheza mechi zao za nyumbani ili kujiweka vizuri zaidi,”
alisema.
Post A Comment: