WATOTO wengi wametajwa kutumia mitandao ya kijamii, kuangalia mambo
ambayo ni kinyume na maadili, jambo ambalo wameaswa kuitumia kujifunza
mambo yenye manufaa kwao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Sihaba Nkinga alisema hayo wakati akifungua mkutano wa tatu wa
kamati kuu ya Baraza la Watoto Tanzania.
Aidha Nkinga aliwataka watoto kuhakikisha wanatimiza wajibu wao na kuacha kulalamikia haki bila kutimiza wajibu.
Alisema ushiriki wa watoto ni moja ya haki tano za msingi kwa watoto
wote, bila kujali tofauti zao na serikali inalipa suala la ushiriki wa
watoto umuhimu wa kipekee katika mipango ya maendeleo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya watoto kutoka
Wizara hiyo, Magret Mussai alisema, mkutano huo wa Baraza la Watoto ni
muhimu na utawasaidia watoto kuangalia mambo yao ikiwemo kuangalia
mikakati wa taifa ya ushirikishwaji wa watoto katika mambo mbalimbali.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: