MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema idadi ya watumishi
hewa katika wilaya hiyo, imeongezeka hadi kufikia 89 wakiwa
wamesababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni moja.
Aidha, Hapi amebaini uwepo wa watumishi vivuli 81 katika kada ya
ualimu na hivyo kutoa siku saba kwa maofisa utumishi wa wilaya hiyo,
kuhakiki watumishi vivuli ili kubaini idadi yao na hasara
waliyosababisha.
Hapi aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jijini Dar es Salaam, na kueleza kuwa awali wakati
akiingia katika ofisi yake wiki iliyopita alikuta kuna watumishi hewa 34
waliokuwa wamesababisha hasara ya Sh milioni 512.
Alisema baada ya kufanya uhakiki zaidi walibainika watumishi hewa
wengine 55 walioisababishia serikali hasara ya Sh milioni 619 na hivyo
kufanya jumla ya hasara kuwa Sh 1,131,754,081.
“Bado uhakiki wa kina unaendelea ili kuhakikisha tunamaliza hili
tatizo la watumishi hewa katika wilaya ya Kinondoni, awali walikuwa 34
lakini sasa wameongezeka 55 na kufikia 89,” alisema Hapi.
Akifafanua kuhusu watumishi vivuli, Hapi alisema watumishi hao ni
wale ambao walihamishwa bila kufuata taratibu na hivyo kuendelea kupokea
mshahara wa kazi yake ya awali badala ya kazi yake mpya.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: