Asilimia 91 ya wananchi waliohojiwa wanaitaka Serikali kabla ya
kukifungia chombo chochote cha habari ni vema kukifikisha chombo hicho
mahakamani ili kutoa fursa ya suala hilo kupitia hatua za kisheria
kuliko ilivyo sasa.
Mapendekezo hayo yametolewa katika ripoti ya utafiti wa wananchi juu
ya haki ya kupata habari iliyofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali ya
TWAWEZA ikionyesha kuwa wananchi wengi wanaunga mkono suala la uwazi na
uwajibikaji na kuwa upatikanaji wa habari huzuia vitendo vya rushwa.
Akiongea wakati wa uwasilishwaji wa ripoti hiyo kwa waandishi wa
habari hii leo jijini Dar es salaam, mshauri mwandamizi wa mawasiliano
wa tasisi ya TWAWEZA Risha Chande amesema,
Takribani wananchi kati ya
wanane na kumi ambao ni sawa na asilimia 78 wanaamini upatikanaji wa
habari unapunguza vitendo vya rushwa, huku wanachi kati ya sita na kumi
ambao ni sawa na asilimia 68 wamependekeza serikali iwe na mamlaka
muhimu ya kuzuia habari zinazotishia usalama wa Taifa.
Aidha, ripoti hiyo pia iligusia hali ya upatikanaji wa habari kutoka
taasisi za umma kwa wananchi ambapo zaidi ya wananchi kati ya wanane na
kumi walio hojiwa katika ripoti hiyo wamesema hawajawahi kufika katika
ofisi za mamlaka ya Maji, shule za Umma, vituo vya Afya wala ofisi za
serikali za mitaa kutafuta taarifa zozote nakuwa wananchi wengi
wakitegemea vyombo vya habari mbalimbali kupata taarifa kutoka taasisi
hizo.
Richa amesmea Redio inaaminika na asilimia 80 ya wananchi, runinga
(TV) inaaminika na asilimia 73 ya wananchi, tofauti na magazeti ambayo
yanaaminika kwa asilimia 27 tu ya wananchi. Japokuwa mitandao ya kijamii
inaaminika kwa kiasi kidogo sana na kutumiwa kwa kiwango cha chini kama
chanzo cha habari.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: