ads

Kiongozi Mwandamizi wa dhehebu la Kiislamu la Shia Ithnashery nchini Tanzania Imamu Swadiq Sheikh Hemed Jalala ameitaka Serikali ya awamu ya tano kuzingatia utawala bora na kuweka usawa baina ya wananchi bila ya kuangalia tofauti zao ili kwa pamoja waeze kujiletea maendeleo.


Sheikh Jalala ameitoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mrithi wa Mtume Muhamad Imam Ali ambae alikufa miaka elfu moja na 30 iliyopita lakini anakumbukwa kwa utawala wake wa kuzingatia usawa kwa binaadamu.

Aidha Sheik Jalala amesema kuwa Utawala bora hauwezi kupatikana kama hakutakuwa na utulivu na amani katika nchi hivyo serikali ya awamu ya tano isimamie kikamilifu suala la amani na utulivu ili wananchi waweze kufanya kazi kwa bidii.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: