KIWANGO cha pensheni kwa wastaafu walio kwenye mifuko mbalimbali ya
hifadhi ya jamii waliokuwa wakilipwa kima cha chini Sh 50,115
kinatarajiwa kuongezwa kwa asilimia 100 hadi Sh 100,125.
Naibu Waziri Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema jana bungeni
kwamba, wastaafu hao wataanza kulipwa kiwango hicho kipya pamoja na
malimbikizo yao baada ya utaratibu unaoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya
Mifuko hiyo (SSRA) kukamilika.
Kijaji alisema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa
Viti Maalumu, Conchester Rwamlaza (Chadema), aliyetaka kufahamu ni lini
wastaafu wataanza kulipwa fedha hizo. Mbunge huyo alisema tangu bajeti
inayoisha ya mwaka 2015/16, serikali kupitia wizara ya fedha iliahidi
kupandisha pensheni kwa wastaafu wanaolipwa Sh 50,000 ili walipwe
100,000.
Alisema ahadi sasa, haijatekelezwa kwa wastaafu hao, jambo linaloleta
usumbufu na wao kushindwa kufahamu ni lini wataanza kulipwa fedha hizo.
Naibu Waziri Fedha na Mipango, Kijaji, alikiri kwamba wastaafu wote
kwenye mifuko wanaolipwa kima cha chini cha pensheni cha Sh 50,000
kuanzia Julai ,2015 walipaswa kulipwa kima kipya.
“Ni kweli serikali ilitekeleza ahadi ya kuongeza kima cha chini cha
pensheni kufikia 100,125.85 kutoka Sh 50,114.43, tangu agizo hilo
lilipotolewa Julai mwaka jana ni Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF) pekee ndio ulioanza kutekeleza agizo hilo kuanzia Julai mwaka
jana,” alisema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: