ads

Serikali imesema kuwa baraza la uwezeshaji Wananchi(NEEC),limeanza kutengeneza utaratibu wa namna ya fedha milioni 50 kwa kila kijiji zitakavyoweza kuwafaisha wananchi wote vijijini wakiwemo Vijana na Wanawake.


Akizungumza  Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa nchini Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Muhagama, amesema fedha hizo zitatolewa kwa kila Mtanzania bila kujali itikadi ya Vyama kama habari ambazo zinasaambaa sasa kuwa watagawiwa wanachama wa CCM, pekee.

Waziri Muhagama, amesema jambo hilo linalozungumzwa ni hofu tu ya baadhi ya watu na kuongeza kuwa serikali itazingatia utaratibu wa kisheria wa kuhakikisha fedha hizo zinawafikia Watanzania wote wanaohusika na mpanngo huo.

Mhe. Muhagama amesema kuwa fedha hizo zilikuwa ni ahadi ya rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kampeni zake ambazo zipo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi lakini haimaanishi kuwa fedha hizo zitagawiwa kwa wanachama wa chama hicho Pekee.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: