ads

 
Chama cha soka nchini Uingereza FA kimebainisha kuwa Jamie Vardy atakosa mchezo muhimu wa klabu ya Leicester dhidi ya Manchester United jumapili ijayo kwa adhabu ya nyongeza ya mechi kutokana na utovu wa nidhamu.


Chama cha soka nchini Uingereza FA kimebainisha kuwa Jamie Vardy atakosa mchezo muhimu wa klabu ya Leicester dhidi ya Manchester United jumapili ijayo kwa adhabu ya nyongeza ya mechi kutokana na utovu wa nidhamu.

Leicester itahitaji kushinda mchezo huo ili kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza lakini kumkosa Vardy huenda ikawa na wakati mgumu.

Mpinzani wa Leicester katika mbio za ubingwa, klabu ya Tottenham imewapa nafasi mbwea hao, baada ya kutoka sare ya 1-1 na Westbrom, na hesabu za ubingwa ni kushinda mechi moja kati ya 3 zilizobaki.

Vardy aliyekuwa mwiba kwa mabeki kwenye msimu huu, alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuzozana na mwamuzi wa mchezo ulioisha kwa sare ya 2-2 dhid ya Westham April 17 mwaka huu.

FA pia imeipiga faini paundi, 20,000 klabu ya Leicester kwa kushindwa kudhibiti wachezaji wake kwa kuonyesha utovu wa nidhamu.
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: