SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo amesema, Halmashauri ya
Jijiji la Dar es Salaam itahakikisha umiliki wa Shirika la Usafiri Dar
es Salaam (UDA) unarudishwa kwa umma,
Tayari ripoti iliyotolewa jana mjini Dodoma na Profesa Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inaeleza hisa za UDA zilithaminishwa kwa bei ya Sh. 744.79 kwa kila hisa Oktoba 2009 na Novemba 2010 thamani ya kila hisa ikiwa Sh. 656.15.
Kulingana na mkataba wa kuwasilisha hisa wa 11 Februari 2011, mnunuzi (kampuni ya Simon Group Limited) alitakiwa kulipa Sh. Bilioni 1.14 kwa bei ya ununuzi wa hisa zote.
Hata hivyo, mnunuzi alilipa Sh. 285 Milioni pekee katika akaunti namba OJ1021393700 ya benki ya CRDB inayomilikiwa na UDA.
Idd Simba, Mwenyekiti wa Bodi alipokea kiasi cha Sh. 320 milioni kupitia akaunti yake binafsi kutoka kwa mwekezaji ambapo kwa mujibu wa Simba, ni ada ya ushauri alioutoa kwa mwekezaji jambo ambalo linaonesha kuwepo kwa mgongano wa masilahi.
Kubenea amesema, “alichokisema
CAG kuhusu UDA kimedhihirisha ambacho tumekuwa tukikisema muda mrefu.
Mchakato mzima wa uuzwaji wa UDA ulikuwa wa rushwa, wizi, udanganyifu na
matumizi mabaya ya madaraka.
“Sisi wabunge wa Dar es Salaam kupitia muungano wetu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) tumedhamiria kuirejesha umiliki wa UDA kwa umma kwa asilimia 100.”
“Tunataka kuona mali zote za UDA zipo wapi? Tumeambiwa hati za UDA zimewekwa benki. Tunataka kujua ni zipi na za gharama gani. Tunamtaka Rais John Magufuli atuunge mkono katika hili,” amesema Kubenea.

DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: