MIONGONI watu maarufu hivi sasa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashiriki katika mtandao wa kijamii wa Twitter ni pamoja na Raid Uhuru Kenyatta wa Kenya ,hii ni kutokan ana kuwa na wafuasi wengi ambao wanamfanya kuwa juu sawa na mastaa wa muziki na filamu.
Moja kati ya tukio ambalo limegonga vichwa vya habari katika mitandao ya kijamii hasa huo wa Twitter ni kitendo cha Kenyatta kuamua ku-unfollow baadhi ya watu mashuhuriakiwemo Makamu wake wa Rais Willium Rutto pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta.
Wengine walioa unfollow na Kenyatta ni msemaji wa Ikulu ya Kenya Manoah Esipisu ,Mkurugenzi mkuu wa Safaricom CEO Bob Collymore,Mkuu wa Jeshi la Polisi Kenya Joseph Boinnet, Katibu mkuu kiongozi wa Kenya (CS) Eugene Wamalwa, Rais wa Afrika Kusini
Jacob Zuma na Rais wa Zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Pamoja na hayo,Kenyatta ameamua kusalia na watu 11 tu ambao ndio amewafollow kupitia ukurasa wake huo wa Twitter ,watu hao ni pamoja na Rais wa Tanzania Dr John Magufuli,Rais wa Marekani Barrack Obama, Rais wa Ufaransa François Hollande ,Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Waziri Mkuu wa Japan Abe Shinzo.
Miongoni mwa viongozi wengine wa Afrika waliosalia katika orodha ya watu 11 wa Kenyatta ni pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Akinwumi A. Adesina.
Miongoni mwa viongozi wengine wa Afrika waliosalia katika orodha ya watu 11 wa Kenyatta ni pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Akinwumi A. Adesina.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: